Thursday, December 26, 2013

klptz

Safari ya miaka  30 ya kanisa la pentekosteTanzania(KLPT)
Mch.DK.Philemon
Tibanenason kuongoza tena KLPT
Na
SalesiMalula
Kanisa la
KLPT linaloongozwanaMchungaji Philemon Tibanenason,limekua likipiga hatua siku hadi
sikuna kufanikiwa kufungua matawi nchini kote na kufanya mambo mbalimbali yakiroho
na kijamii pia.
Mchungaji  Mchungaji job sembuche nikatibu mkuu wa kanisa
hilo ambaye alitoa taarifa juu ya upentekoste na kanisa hilo ambapo alisema:
“Ukweli nikwamba
tunapozungumzia Kanisa la PentekosteTanzania(KLPT)hatuwezi kuacha kuunganisha historia
ya upentekoste hapa nchini.Lakini piahuwezi kuelewa mwanzo wakanisa la
Pentekoste Tanzania nje ya historia nzima ya upentekoste.
Historia ya Upentekoste
hapa Tanzania ilianza mwaka 1913 ambapo wamissionari wa kipentekoste Karl,marian
wittik na Clarence Grothaus kutoka sweeden,waliingia Itigi Mkoani Singida ambapo
walichukua muda mfupi na kuelekeaTabora eneo la Tazengwa.
Mwaka 1949
wamissionari kutoka sweeden walikuja Jijini Dar essalaam kuanza kazi ya Mungu ambapo
walipofika tu walipewa nyumba ya kuishi katika majengo ya nyumba ya sanaa karibu
na Serena Hotel na wamissionari hawa walikuja chini ya Kanisa la Sweedish Free
Mission.
Haikuwa rahisi
kwao kuanzisha kazi katika maeneo ya Upanga kwani waliona eneo hilo liko mbali na
makazi ya watu.
Mwaka 1952
waliomba kuhamia maeneo ya Ilala Boma ambako walifanikiwa kuanza kazi ya Mungu na
kufanikiwa kujenga kanisa ambapo waanzilishi wa Kanisa hilo ni Mchungaji Ernest
Nikwisto na kazi hii ilikuwa chini ya kanisa la Philadephia scothom.
Akifafanua zaidi
katibu mkuu huyo anasema mwanzoni mwa mwaka 1960 kulikua na uamsho mkubwa wa wahindi
ambao walikua wakipinga injili kuhubiriwa ambapo walikuwa wakIsema hata kwaupanga
injili haitaweza kuhubiriwa hapo ndipo neno “Upanga” likazaliwa na kushika hatamu
hadi hivi leo.
Akichambua zaidi
Mchungaji Sembuche anasema kutokana na vuguvugu la uhuru wa Tanganyika kushika kasi
baadhi ya wamissionari waliondoka kutokana  na hofu ya mambo yatakuwaje,na baadaye wachungaji kadhaa waliitwa ilikusaidia
kazi hapa Jijini Dar essalaam.ambapoMchungaji Hassan Lolo kutoka Congo,Adonia Balishikwa
naMchungaji Harris Kapiga walikabidhiwa kazi.
Mwaka 1967
Mmisionari Oscar Langestrom na mkewe Martha wakawa na maono ya kituo cha
maandiko ambapo walinunua jingo lililopo Mtaa wa (Lindi sofia kawawa) mahali ambapo
leondipo lilipo Jengo la Kanisa la KLPT Parishi ya Jiji(City parish)
linaloongozwa na Mwangalizi Mkuu wa kanisa hili hapa nchini Mchungaji Philemon
Tibanenasoni.
Baadaye wamisionari
hawa walimkaribisha Mchungaji Simon katete kutoka Bigabiro Kigoma ili kusaidia kazi
ya Mungu iliyokuwa imeanza hapo Lindi Street ambapo kanisa lilikuwa na waumini
10 na halikuwa na wazee wa Kanisa wala Mashemansi, kutokana na ugumu wakazi hiyo
ilibidi Mchungaji Simon kakete akawashauri wamisionari wamuite Mchungaji
Philemon Tibanenason na mkewe Juliana Tibanenason waliokuwa watumishi wa Kanisa
la Bukoba.
Oktoba 10
mwaka 1969 Mchungaji Dk.Philemon Tibanenason na mkewe waliingia jijini Dar es
salaam kuja kuanza kazi rasmi
Kanisa la
Pentekoste Dar essalaam
Mwaka
1971,wamisionari waliandikisha kanisa kwa jina la “Kanisa la Pentekoste Dar es
salaam” kutoka Sweedesh  Free Mission
nakuweka wadhamini ambaoni wazalendo waliochaguliwa na missionari nao ni Aron Mabondo
marehemu, matusela majige marehemu,Herman Rwekamwa marehemu na GelsonRioba.
Tarehe 12 December
1972 Mchungaji Dk.Philemon Tibanenason na marehemu Aron Mabondo waliwekewa mikono
kuwa wazee wa kanisa,na siku hiyo hiyo wamisionari wakamuwekea mikono Dk.Philemoni
na mkewe kuwa wachungaji.
Sembuche anasema
Dk.Philemon Tibanenason akaanza kazi ya waumini 10 huku viti zaidi ya 400
vikiwa tupu.
Anasema tangu
siku hiyo uamsho mkubwa ulianza kutokea katika kanisa hilo, na miaka iliyofuata
ilikua ni ya uinjilisti wenye nguvu ukiambatana na udhihirisho wa nguvu za Mungu
huku wenye magonjwa wakifunguliwa mara baada ya maombezi.
Kulikua na uamshom
kubwa katika maeneo ya Kisarawe, ,lindi, Rufuji, Bagamoyo, Mbeya na Zanzibar, Kutokana
na kanisa kuwa na Exemption Certificate liliruhusiwa kuhubiri sehemu mbalimbali
kama vile;Morogoro,Bukoba,Singida,Kilimanjaro, na Arusha ambapo kanisa la
Pentekoste Dar es salaam lilikuwa na matawi nane yaani Dar essalaam, Pwani,Lindi,Mtwara,Unguja
Kaskazini, Ruvuma, Mbeya na Iringa.
Mwaka 1979
Serikali ilitoa ushauri kanisa litoke kwenye exemption ili liweze kuendana na kasi
ya kazi linayoifanya ikiwepo kubadilisha jina la kanisa ambapo katika upelekaji
injili kanisa liliweza kukumbana na changamoto kubwa katika kuipeleka injili kwani
jina lilionekana ni kanisa la Dar es salaam tu hivyo ikawa kikwazo kikubwa cha
kuipeleka injili.
Tarehe 23
march 1983 Mkutano Mkuu waKanisa la  Pentekoste Dar es salaam ulikaa na kuamua
kubadilisha jina likaitwa Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT) ambapo ulianzisha
Mfumo wa majimbo na Parish ambapo kikao kiliamua matawi yote yaKanisa la
Pentekoste Dar es salaam kuwa maparish ya kanisa la Pentekoste Tanzania.
Baada ya hapo
mchakato wa kusajili Kanisa ulianza ikiwa ni pamoja na kuandaa Katiba mpya na
tarehe 20 May 1992 ililisajiwa rasmi Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT),nakupewa
cheti cha usajili namba SO6649 na huondio ukawa mwanzo wa kanisa la Pentekoste
Tanzania.
Maendeleokwasasa
Kanisa limepiga
hatua kubwa kwani kutoka parish Nane za Kanisa la pentekoste Dar essalaam sasa lina
parish 240 na majimbo 30 nchini kote.
Idadi ya wakristo
imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na mahubiri ambayo huendeshwa na watumishi
kutoka maeneo yote Tanzania.
Sembuche anasema
kanisa limepiga hatua kwa kuanzisha chuo cha Biblia kilichopo nyanda za juu kusini
ambacho kinatoa mafunzo kwa watumishi ya cheti na Stashahada.
Sembuche anasema
bado kanisa limepanua wigo kwa kufungua kazi katika mataifa mbalimbali ambapo limefanikiwa
kufungua makanisa nchini Malawi katika mji wa Chitipa,India katika jimbo la Vijawalda
Andra pradesh.
Katika mkutano
huo Mkuu Kanisa limeamua tena kumchagua Mchungaji DK.philemon Tibanenasoni kuliongoza
Kanisa hilo kwa muda wa miaka kumi ijayo.
Tibanenason ameliongoza
kanisa tangu mwaka 1992 alipochaguliwa hadi hivi leo.
Akitoa shukurani
zake mbele ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo mkuu DK.Tibanenason anasema katikamiaka
10 ijayo vipaumbele katika kanisa lao ni kufanya kampeni maalumu ya uinjilisti katika
maeneo ya vijijini,kuimarisha huduma ya maombi na maombezi kwa ajili ya taifa
la Tanzania,kuweka mkazo katika eneo la utoaji wa mafundisho sahihi kwa kanisa,
kuhimiza Elimu yam Biblia,ikiwa ni kuweka mkazo na kuwahimiza wachungaji kwenda
kusoma,kutoa kipaumbele katika masula ya elimu kwa kujenga shule ya msingi,sekondari
hadi chuo kikuu, kuimarisha uchumi wa kanisa, kuanzisha vyombo vya habari vya kanisa
pamoja na ujenzi wa hospitari kwa manufaa ya jamii nzima ya watanzania bila
kujali utiofauti wa imani zetu.
Amewaomba wajumbe
kudumisha umoja na mshikamano ili kazi ya Mungu iweze kusonga mbele na amewahakikishia
wajumbe kuwa vipaumbele vyakanisa vilivyopendekezwa atavifanyia kazi ili kufikia
malengo kwa manufaa ya kanisa na taifa kwa ujumla.

6 comments:

  1. Nataka kufahamu mwendelezo wa utumishi wa mchungaji Harris kapiga baada ya kukabidhiwa kazi mwaka 1967

    ReplyDelete
  2. Ameeeeeni ninashukuru sana kuijua historia hii

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Elezea vizuri hiyo histori unaficha mambo mengine utahukumiwa

      Delete
    2. Nikusaidie Mchaji,Swedish Free Mission ilikuwa na mfumo huu,kila kanisa la mahali ilikuwa na usajili wake na ndio maana lilisajiliwa kwa Kanisa la pentekoste Dar Es salam walikuwa mfumo wa local church.Kanisan la Klpt lilijitenga mwanzilishi ni mtoto wa Adrea shimba(Uongo unaotumia utahukumiwa.Klpt,Fpct,mmpt yote yametokana na(Kanisan la Pentekost)walioiacha Swedish Free mission

      Delete
  4. How to make a titanium money clip in a slot machine
    A slot machine is titanium price per pound a type of machine machine made by the makers of slots. It consists of titanium gr 2 a spinning reel, camillus titanium knife a oakley titanium sunglasses spinning raw titanium ball, and a revolving

    ReplyDelete